October 18, 2019


IVAN Rakitic, kiungo wa Barcelona amesema kuwa anachoshwa na kuanza kuwekwa benchi na kukosa muda wa kucheza.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 31 alikuwa chaguo la kwanza la Kocha Ernseto Valverde, kwa sasa ameanza kupata wakati mgumu kupata namba kutokana na uwepo wa Frenkie de Jong.


 "Ni wakati mgumu kwa kuwa ninataka kucheza na siyo kuwa sehemu ya timu.

 "Nitapambana kufanya inavyowezekana, bado nina mkataba wa miaka miwili na kwa sasa hakuna sehemu bora kama Barcelona,".

 Rakitic amecheza jumla ya mechi 274 na kutupia mabao 34 katika miaka mitano aliyoitumikia timu hiyo tangu alipojiunga 2014 akitokea Sevilla.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic