October 22, 2019


Arturo Vidal ndiye jina lake mwaka Jana, Oktoba aliwekwa benchi dhidi ya Tottenham Hotspur kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hakuwa na furaha kabisa Kwa kuingizwa dakika nne za mwisho kabla gemu kuisha.

Ameletwa duniani Mei 22,1987 ana urefu wa futi 5 inchi 11 anakipinga ndani ya Barcelona. Mwili wake mkubwa umejawa na michoro ambayo kila kona akiwa uwanjani ni mtu wa kazi.

Wengi waliamini kwamba kitendo chake cha kuposti kikatuni cha sura iliyokasiriki kwenye mitandao ya kijamii kungemfanya nyota huyo kusepa ndani ya Barcelona.

Bado anakipiga Barcelona kwa sasa ambayo ina kibarua cha kutetea taji lake la La Liga msimu huu ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 19 baada ya kucheza michezo tisa, kesho itakuwa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Slavia Praha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic