MABONDIA wa
ngumi za kulipwa nchini, Issa Nampepeche na Ally Hamisi wanatarajia kupima
uzito leo tayari kwa pambano la usiku wa mabingwa litakalofanyika Oktoba 4,
mwaka huu kwenye Ukumbi wa Club 361 uliopo Mwenge, Dar.
Mbali
ya mabondia hao wengine watakaopima uzito kwa ajili ya pambano hilo ni Said Sudi atakayezichapa na Maganga Kulwa,
Ibrahim Makubi dhidi ya Abdallah Kingolwira, Hashimu Msungo vs Epson
Lewis wakati Salumu Omari atamalizana na Ramadhani Chicho yakiwa
chini ya udhamini wa Gazeti la Championi, +255 Global radio, Smart
Gin, Glady Matata na Kiwango Security.
Mratibu
wa pambano hilo, Seleman Semunyu ameliambia SpotiXtra kuwa maandalizi ya
kuelekea katika pambano hilo yamekamilika ambapo leo mabondia wanatarajia
kupima uzito kwenye Ukumbi wa Club 361.
“Maandalizi yanakwenda vizuri kwa mabondioa
wote ambao watapanda ulingoni siku hiyo ambayo itakuwa ni kazi moja tu ya
kuwapongeza mabondia wetu ambao wamechukua mikanda ya ubingwa nje ya mipaka ya
Tanzania.
“Uzito tumepanga wapime Alhamis (leo) kabla ya siku ya Ijumaa ambayo mabondia
wenyewe ndiyo watapanda ulingoni, kikubwa mashabiki wa mchezo wa ngumi za
kulipwa wajitokeze kwa wingi siku hiyo kushuhudia ngumi zikifanyika katika ustarabu
wa hali ya juu kwa kiingilio kidogo,” alisema Semunyu.
0 COMMENTS:
Post a Comment