October 12, 2019


Jose Mourinho amekataa ofa ya kuifundisha klabu ya Lyon kwa kuwa ameshapata klabu nyengine, hayo ni kwa mujibu wa rais wa ligi ya Ufaransa, Jean-Michel Aulas. (Goal)

Manchester United inajipanga kulipa kitita cha pauni milioni 130 kuwanyakua wachezaji wawili wa Leicester na England; mlinzi Ben Chilwell na kiungo James Maddison, wote wana miaka 22. (Sun)

Hata hivyo kuna ripoti zinadai kuwa klabu ya Chelsea kwa sasa ndio wanapigiwa upatu zaidi kumnasa beki wa kushoto Chilwell pale marufuku dhidi yao ya usajili itakapokwisha. (Mail)

Manchester United wanataka kusajili wachezaji wapya nane katika kipindi cha misimu miwili ijayo na tayari wameshaandaa orodha ya wachezaji hao. (Telegraph)

Real Madrid hawataki kupoteza bahati kwa kutomsajili kiungo wa Denmark Christian Eriksen, 27, mpaka mwisho wa msimu ambapo kuna uwezekano akaongeza mkataba na klabu yake ya Tottenham. (Marca)

Tottenham pia wana matumaini kuwa watamuuza Eriksen mwezi Januari tili kuzuia wasimpoteze bure mwishoni mwa msimu ambapo mkataba wake utakuwa unaisha. (Mirror)

Japo rais wa Real Madrid Florentino Perez anataka kumsajili Eriksen, kipaumbele cha kocha Zinedine Zidane bado ni kiungo wa Manchester United Paul Pogba, 26. (ESPN)

Manchester City wanatafakari juu ya kufanya usajili wa mwezi Januari kwa kumnunua beki wa timu ya Benfica Ruben Dias, 22, ambaye pia anahusishwa na uhamishi kuelekea Manchester United. (Mirror)

Arsenal wapo katika mazungumzo na klabu ya Uturuki Fenerbahce juu ya usajili wa mkopo wa kiungo Mesut Ozil, 30. (Takvim - in Turkish)

Kocha wa Everton Marco Silva amepewa michezo mitatu ya kubadili hali ya mambo ama atimuliwe kazi. (Star)

Beki wa Barcelona Gerard Pique, 32, alikaribia kuinunua klabu ya Notts County mwishoni mwa msimu uliopita. (ESPN)

Kocha wa Juventus Maurizio Sarri anataka kumsajili beki wa kushoto Mtaliano Emerson, 25, kutoka Chelsea. (Express)

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic