October 20, 2019


Mesut Ozil amesisitiza kuwa ataendelea kuitumikia timu hiyo hadi mkataba wake utakapomalizika hata kama hatakuwa akipata nafasi ya kucheza.

Kwa kauli hiyo pekee inamaanisha kuwa hadi mkataba wake unamalizika atakuwa ameingiza pauni 31m hata kama atakuwa hachezi.

Kiungo huyo raia wa Ujerumani analipwa pauni 350,000 kwa wiki, amekuwa hana uhakika wa namba chini ya kocha wake wa sasa, Unai Emery.

Arsenal ilitaka kumuuza katika usajili uliopita lakini ikashindikana kutokana na dau lake kubwa la mshahara, pamoja na hivyo bado klabu hiyo ina mpango wa kumuondoa katika usajili mdogo wa Januari, mwakani.

Kwa maana hiyo, Arsenal wanatakiwa kupata timu ambayo itakuwa tayari kumlipa mshahara anaotaka Ozil, kinyume na hapo ni wataendelea kumlipa hadi mwaka 2021 wakati mkataba wake utakapomalizika.

Hadi sasa kwa msimu huu Mjerumani huyo ameshiriki katika michezo miwili kati ya 11 huku akiwa ameachwa katika michezo mitatu iliyopita.

Michezo ambayo Ozil alionekana ni dhidi ya Watford katika Premier League na dhidi ya Nottingham Forest katika Carabao Cup. Tangu kuanza kwa msimu huu hadi sasa kiungo huyo wa zamani wa Real Madrid ameshaingiza benki pauni 3.15m kutokana na mshahara anaolipwa

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic