MKUDE CHAMA KUKATWA MPUNGA SIMBA
Baada ya kutuhumiwa kuwa walikuwa na makosa ya kinidhanu, inaelezwa wachezaji Gadiel Michael, Jonas Mkude, Erasto Nyoni na Clatous Chama walifikishwa kwenye kamati ya nidhamu.
Taaifa zimeeleza kuwa CEO mpya wa klabu hiyo, Senzo Mazingiza, amesema tayari walikutana na wachezaji hao na tayari wameshamaliza.
Bosi huyo amefunguka kuwa kuna mambo hayakuwa sawa na upande wao kama uongozi waliamua kukaa nao kikao kwa ajili ya kuyamaliza.
Hata hivyo, taarifa imesema kuwa Mazingiza ameeleza wachezaji hao wanne wataendelea na kazi kama kawaida lakini kuna adhabu ambazo watapewa huku wakiendelea na kazi.
Taarifa zilizo chini ya kapeti zinasema uwezekano wa kukata baadhi ya fedha zao unaweza ukafanyika.
Kwa hiyo inatuhusu nini mwandishi?....kwani wewe ukifanya kosa kazini unatujulisha kuhusu adhabu uliyopewa?...tuletee habari zenye mantiki chanya sio za unafiki-unafiki.
ReplyDelete