October 26, 2019


Kuelekea mechi ya Simba dhidi ya Singida United Jumapili ya wiki hii, Mkurugenzi wa Singida, Festo Sanga, amewapiga mkwara wapinzani wake kwa kusema watawasimamisha kuendelea kubeba alama tatu.

Sanga ameeleza kuwa wamejipanga vilivyo kuhakikisha wanatwaa alama hizo tatu mbele ya Simba ambao ni vinara wakiwa na alama 15 mpaka sasa.

Kiongozi huyo amesema msimu haujawa vizuri kwao kutokana na timu yao kushika mkia kwenye ligi hadi sasa.

"Sisi tumejipanga na tupo tayari kuchukua alama tatu za Simba.

"Tumejiandaa vema zaidi, mashabiki wasubirie tu dakika 90, naamini tutapata matokeo.

"Mashabiki waje kwa wingi ili kutoa sapoti kwani itakuwa chachu ya kupata matokeo."

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic