ZIDANE MAJI YA SHINGO MADRID
Kitendo cha Real Madrid kupata sare tena ya kuitafuta kwa ‘tochi’ dhidi ya Club Brugge ya Ubelgiji katika Ligi ya Mabingwa Ulaya sasa ni rasmi kimemuweka pabaya Zinedine Zidane.
Real Madrid, mabingwa mara 13 wa michuano ya Ulaya walipata sare ya mabao 2-2 wakiwa nyumbani dhidi ya timu ambayo ilionekana ni ndogo kwao, kitendo ambacho kimewachukiza mashabiki wengi wa Madrid na kuamini kocha wao, Zidane sasa timu imemshinda.
Sawa na Polisi kupata Sare na Wananchi!
ReplyDelete