October 30, 2019





FT: Mwadui 1-0 Simba

Uwanja wa Kambarage

Mchezaji wa Mwadui FC anatolewa nje kwa machela 

Mashabiki wa Simba wanaanza kuondoka uwanjani

Zinaongezwa dakika tano

Dakika ya 90 bado ngoma ni 1-0  Dakika ya 80 Mwadui wanaliandama lango la Simba kwa pasi zenye macho Dakika ya 78 Ajibu anapiga kona ngoma inaokolewa na mlinda mlango wa Mwadui Dakika ya 76 Ajibu anapaisha faulo
Dakika 75 Agustino Samson anaonyeshwa kadi ya njano
Dakika ya 75 Miraj anachezewa rafu
Dakika ya 74 Manula anaanzisha mashambulizi kwenda kwa Mwadui ila mpira unatolewa nje unarushwa kwenda kwake tena
Dakika ya 73 Nyoni anacheza rafu kwa mchezaji wa Mwadui
Dakika ya 71 Mahamoud Amir mlinda mlango wa Mwadui anaonyeshwa kadi ya njano
Dakika ya 68 Ajibu anapiga kona haizai matunda
Dakika ya 66 Mlinda mlango wa Mwadui yupo chini akipatiwa huduma ya kwanza
Dakika ya 65 Ajibu anapiga kona hekaheka ndani ya lango mpira unaokolewa na refa nasema mlinda mlango amechezewa rafu.
Dakika ya 64 mchezaji wa Mwadui amenguka anabebwa na machela kutolewa nje
Dakika ya 63 MK 14 anapambana ndani ya 18 ngoma inatoka nje na mlinda mlango anaokoa 
Dakika ya 62 Dilunga anapiga pasi ndefu inaokolewa kimaajabu na beki wa Mwadui kwa kichwa
Dakika ya 61 pasi ya Ajibu inamkuta Miraj anaokolea nje ya uwanja Dakika ya 60 Ajibu anaingia anatoka KahataDakika ya 58 mpira umesimama kuna mchezaji wa Mwadui ameanguka, Ajibu anaongea na Mbelgij ili afanyiwe mabadiliko
Dakika ya 57 Miraj anapiga pasi ndefu inayokoswa na KahataDakika ya 56Mwadui wanakosa nafasi ya wazi kabisa ndani ya 18, ngoma imezidi kuwa ngumu kwa Simba leo
Dakika ya 55 Gadiel anarusha mlinda mlango anadaka, ngome ya Mwadui ipo imara, mpira kwa Simba hautulii kabisa leo, 
Dakika ya 54 Mwadui wanawachezea Simba kama wanavyotaka, Miraj, Dilunga ngoma inaokolewa na beki wa Mwadui. Gadiel anarusha mlinda mlango Mahamoud anadaka
Dakika ya 53 mlinda mlango wa Mwadui anajitoa langoni na kuokoa hatariDakika 52 Kahata anapoteza mpira ndani ya 18 Dakika ya 51 Mzamiru anampa Gadiel anatoa nje
Dakika ya50 Geral anaisumbua safu ya ulinzi ya Simba
Dakika ya 49 mshambuliaji wa Mwadui anakosa nafasi ya waziDakika ya 48 Gadiel anachezewa rafu
Dakika ya 47 Shamte anapiga free kikc haina matunda
Shiboub nje anaingia Dilunga, Chama nje ndani Miraji dakika ya 45

Meddie Kagere na Joram wanaonyeshwa kadi ya njano dk ya 45.
Bao la kuongoza kwa Mwadui FC lilifungwa na Gerland dakika ya 32

Mpira kwa sasa uwanja wa Kambarage ni kati ya Mwadui FC na Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara.

Mwadui FC wapo mbele kwa bao 1 kwa sasa ni mapumziko.

Mashabiki wamejitokeza kwa wingi kushuhudia kandanda hili hapa  kwenye uwanja wa Kambarange Shinyanga

3 COMMENTS:

  1. Ndio kawaida ya matokeo ya soka kufunga,kufungwa ama kutoka sare.Japo ligi bado mbichi lkn kipa Manula mhhhh

    ReplyDelete
  2. Leo ndio mnasema kawaida ya matokeo!

    ReplyDelete
  3. We ulitaka asemeje tumefungwa kiuchawi,tatizo la wabongo Simba ikifungwa inaonekana kama maajabu saba ya dunia,pambaneni na hali zenu Simba wanaongoza ligi na ndo timu inayopewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa tuombe uhai

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic