NAMNA HALI YA BOCCO ILIVYO SASA
Baada ya kuanza mazoezi mepesi siku kadhaa zilizopita, straika wa Simba, John Bocco bado hajaungana na wenzake katika mazoezi ya pamoja kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara.
Bocco ambaye aliumia miezi kadhaa iliyopita na hadi sasa hajacheza mchezo wowote wa ligi, anaendelea na ratiba binafsi ya mazoezi kwa ajili ya kujiweka fiti.
Taarifa zinaeleza kuwa Bocco hali yake haijaimarika kiasi cha kufikia hatua aungane na wenzake mazoezini kwa ajili ya kujifua.
Licha ya kutoanza mazoezi na wenzake, taarifa zinasema maendeleo ya mchezaji huyo aliyewahi kuichezea Azam yanaenda vizuri na kuna uwezekano anaweza kuwa sehemu ya kikosi siku za usoni.
Tangu Bocco aumie, Simba ipo nafasi ya kwanza kunako msimamo wa ligi ikiwa na alama 12 ikiwa imecheza jumla ya mechi nne ilizoshinda zote.
Enter your comment...asante sana kwakutujuza
ReplyDelete