October 23, 2019


Kuna uwekezekano mkubwa mfumo wa maamuzi wa VAR (Video Assistant Referee) ambao unatumika katika ligi kubwa za Ulaya ikiwemo England, Hispania na Italia, ukatumika kwenye mechi ya Yanga Vs Simba Januari 4, mwakani.

Mipango hiyo inaendelea kusukwa kwa sasa kwa ajili ya VAR ambayo imekuwa ikiainisha makosa ambayo mwamuzi wa kati hayaoni, kutumika katika pambano hilo ambalo huteka hisia za mashabiki wengi Tanzania.

Timu hizo mbili kwa mara ya kwanza zitakutana Januari 4, kwenye mechi ambayo inasubiriwa kwa hamu na mashabiki wote kutokana na vikosi hivyo kila kimoja kufanya marekebisho makubwa.

Taarifa za ndani kutoka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ambazo Championi Jumatatu limezipata na kuthibitishwa na katibu wa shirikisho hilo, Wilfred Kidau ni kuwa kwa sasa kuna mazungumzo ambayo yanaendelea kwa ajili ya VAR kutumika katika mechi hiyo ambayo itapigwa Uwanja wa Taifa ambao una uwezo wa kubeba mashabiki 60,000.

“Bado hatujakubaliana ila kuna mazungumzo yanaendelea na Simba na Yanga kwa ajili ya VAR kutumika kwenye mechi yao.

“Muelekeo hadi sasa ni mzuri na hiyo itakuwa katika mechi zote za timu hizo zitakapokutana ikiwa ni kujaribu juu ya mfumo huo hapa nchini.

“Kuna uwezekano wa klabu hizo kukubali juu ya mfumo huo kwa ajili ya kuondoa utata wowote utakaojitokeza kwenye mechi hiyo.

“Ingawa haijathibitishwa kwa asilimia 100 lakini tunafikiria VAR itakuwepo katika mchezo huo na itatumika kwa majaribio japokuwa hatujajua huko mbele itakuwaje ila tutaanza kuitumia kwa majaribio katika mechi hiyo,” alisema Kidau.

CHANZO: CHAMPIONI

1 COMMENTS:

  1. Mechi ya simba na yanga siyo ya kufanyia majaribio mfumo . Fanyia majaribio mechi ya Gwambina vs ihefu na mafanikio yatakapopatikana ndipo ukatumie katika mechi ya Simba vs Yanga

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic