October 4, 2019


Mshambuliaji wa timu ya Simba ya Dar es Salaam, Miraji Athumani amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa mwezi Septemba wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2019/20, huku Patrick Aussems pia wa Simba akichaguliwa Kocha Bora wa mwezi huo.

Miraji na Aussems walitwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda wenzao walioingia nao fainali katika uchambuzi uliofanywa Dar es Salaam wiki hii na Kamati ya Tuzo ya VPL inayotolewa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kutokana na mapendekezo kutoka kwa makocha waliopo viwanja mbalimbali, ambavyo ligi hiyo inachezwa msimu huu. 

Kwa mwezi huo wa Septemba, Simba ilicheza michezo mitatu na kushinda yote ikiifunga Mtibwa Sugar mabao 2-1, Kagera Sugar mabao 3-0 na Biashara United mabao 2-0, ambapo Miraji alikuwa na kiwango kizuri uwanjani kwa mwezi huo akichangia kwa asilimia kubwa mafanikio hayo ya Simba ikiwa ni pamoja na kufunga mabao mawili na kutoa pasi za mabao mawili. 

Miraji aliwashinda Meddie Kagere wa Simba aliyetoa mchango mkubwa pia katika mafanikio ya Simba ikiwa ni pamoja na kufunga mabao manne.

Mchezaji mwingine aliyeingia fainali alikuwa Ismail Kada wa Prisons aliyeonesha kiwango kizuri na kutoa mchango katika michezo ambayo Prisons  ilicheza ikishinda miwili, sare mmoja, ambapo iliifunga Ruvu Shooting mabao 2-1, Mtibwa Sugar mabao 3-1 na kutoka sare na Lipuli mabao 2-2.

Kwa kutwaa tuzo hiyo, Miraji atazawadiwa kikombe na Tsh. 1,000,000 (milioni moja) kutoka Vodacom. Vilevile atapata Kisimbusi  kutoka Azam TV.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic