October 17, 2019



Kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Etienne Ndayiragije huenda akawa na wakati mgumu kutokana na aina ya matokeo ambayo timu hiyo imekuwa ikipata tangu aanza kuinoa kwa kushindwa kupata ushindi ndani ya dakika 90 kwenye mechi sita.


 Stars juzi Jumatatu iliendelea kushindwa kutamba baada ya mbele ya Rwanda baada ya kuambulia suluhu pale Kigali Rwanda ukiwa mchezo wa kirafiki wa kalenda ya Fifa.


  Mrundi huyo ameisimamia Stars kwenye michuano tofauti kwa dakika 540, ambazo sawa na mechi sita baada ya kuchukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mnaigeria Emmanuel Amunike.


Katika mechi hizo ambazo amesimamia kocha huyo kwenye mashindano tofauti ndani ya dakika 90, hakuna mchezo hata mmoja ambao aliondoka na ushindi.


Mrundi huyo ameisimamia Stars katika mechi sita ndani ya dakika 90 licha ya  kushindwa kuibuka na ushindi lakini  ndani ya dakika hizo yalifungwa mabao mawili pekee na wakiruhusu  mabao matatu.


Kocha Ndayiragije tangu apewa timu hiyo amesimamia mechi zifuatazo; Stars 0-0 Kenya, Kenya 0-0 Stars. Burundi 1-1 Stars, Stars 1-1 Burundi, Stars 0-1 Sudan na Rwanda 0-0 Stars.


MECHI 6:
Mabao ya kufunga 2
Mabao ya kufungwa 3
Ushindi dk 90 hakuna

Kupoteza    mechi 1

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic