SALEH ALLY AZIDI KUICHAMBUA YANGA, AHOJI BALINYA KUKAA BENCHI
Bado Yanga haijafanya vizuri hasa katika Ligi Kuu Bara. Wakati mwingine huwa nafikiri 'approach' ya Ligi ya Mabingwa na Ligi Kuu Bara kwa pamoja kama wameshindwa kudhibiti presha.
Ishu ya kusema hawana wachezaji naona kama ni mapema sana.
Mfano hawa wachezaji WAWILI, Juma Balinya na Papy Sibomana WANA KITU. Lakini kumekuwa na HARAKA sana kuhusiana na hawa lakini wachezaji wengine WANAVUMILIWA na uwezo angalau unaanza kuonekana.
Wakati mwingine mambo ya soka ni process, au hatua. Si kila kitu kinajulikana baada ya mechi moja, au kinafanikiwa baada ya michezo miwili.
Vizuri wao pia waendelee kucheza tena na tena, angalau WAHUKUMIWE kwa mechi za kutosha.
Balinya ni mfungaji Bora Uganda, haiwezekani akawa hajui kufunga. Hivyo apewe nafasi kwa kuwa hawezi KUFUNGA AKIWA BENCHI.
Mfano kama David Molinga "Falcao' alianza na kiwango cha chini, akarudishwa na kupewa mazoezi maalum na akapewa nafasi na kuvumilia, angalau kaonyesha anaweza kufanya kitu.
Kama Balinya ana upungufu, basi ufanyiwe kazi na apewe nafasi. Top scorer vipi akae benchi?
Kumbukeni, haraka kupitiliza mwisho wake ni KUISHIA NJIANI.
Imeandaliwa na Saleh Ally
Watani mnatakiwa kuwa watulivu sana hasa wakati huu wa ligi na kombe la shirikisho msianze kuzozana na maneno yasio kuwa na matokeo.All the best katika mechi yenu na Pramid
ReplyDeleteUnaichambua Yanga kwa kutegemea mawazo ya Mzee Akilimali!!
ReplyDeleteAndiko lako ni zuri sana na lina kitu ndani yake, kama ukiangalia kiundani Yanga kuna tatizo la head coach kuamua anavyoona yeye kuhusu wachezaji fulani.
ReplyDeleteTatizo watu wakisema ukweli inaonekana kama wanaisema vibaya timu lkn ukweli kuna tatizo liko ndani ya kocha lkn wengi hawalioni kwa haraka.
Mzee Akili mali anaamini wachezaji wamelogwa anataka wapapasiwe matunguli kwanza la sivyo Yanga itashuka daraja msimu huu.
ReplyDeleteAnayesema wanelogwa hajui mpira.Nikolas pepe aliyesajiliwa na Asernal nani anamloga? Hajafunga Bado wakati kule alifunga goli 22
ReplyDelete