October 21, 2019


Taarifa zilizopo hivi sasa ni kuhusiana na kiungo fundi wa AS Kigali ya Rwanda, Haruna Niyonzima anatajwa kurejea Tanzania.

Tetesi zilizo chini ya kapeti zinaeleza kuna uwezekano akarejea kunako timu za Simba ama Yanga kwa ajili ya kutoa huduma yake.

Licha ya Simba kumuacha, inaelezwa kiwango alichonacho kiungo huyo hadi sasa kinawavutia kutokana na juhudi zake uwanja.

Niyonzima aling'ara zaidi katika mechi ya kirafiki ambayo Tanzania ilicheza na Rwanda katika mechi ya kirafiki iliyokuwa ni ya kalenda ya FIFA.

Yanga wananyatia kwa nguvu haswa mara baada ya kukutana na bosi wake wa zamani Bin Kleb siku walipocheza dhidi ya Tanzania.

Dirisha dogo kunako Ligi Kuu Bara litafunguliwa Novemba 15 hadi 25.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic