October 4, 2019


DONALD Ngoma, mshambuliaji wa zamani wa Yanga anayekipiga Azam FC ametumia jumla ya dakika 540 kufunga bao lake la kwanza kwenye mechi za ushindani.

Azam FC iliyo chini ya Etienne Ndayiragije imecheza jumla ya mechi sita za ushindani sawa na dakika 540 kwenye michezo hiyo Ngoma hakufunga.

Ilianza kwenye Kombe la Shirikisho ilipocheza na Fasil Kenema ya Ethiopia mchezo wa kwanza ilipoteza kwa kufungwa bao moja kabla ya kupindua meza kibabe kwa ushindi wa mabao 3-1.kabla ya kupambana na Triangle United, ilipoteza nje ndani kwa kufungwa jumla ya mabao mawili 

Mchezo wa tano ilikuwa dhidi ya KMC huu ulikuwa wa ligi na ilishinda bao 1-0 hakufunga bao uwanja wa Uhuru bao lilifungwa na Idd Seleman.

Juzi kwenye uwanja wa Azam Complex Ngoma aiifunga bao lake la Kwanza kwenye mechi za ushindani msimu huu wakati timu yake ikiifunga Ndanda FC mabao 2-0.
.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic