October 20, 2019


Baada vya kufanya vibaya katika msimu uliopita wa Ligi Kuu ya Wanawake bara, Kocha Mkuu wa Yanga Princess, Edna Lema ametamba kufanya vizuri katika ligi hiyo baada ya kusajili wachezaji tisa wapya.

Ligi hiyo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Oktoba 26, mwaka huu, ambapo Yanga itavaana na timu ya baobab Queens ya Dodoma katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Kocha Edna ameliambia Championi Jumamosi kuwa, usajili walioufanya kuelekea msimu huu wa ligi hiyo umezingatia mahitaji ya timu hivyo wanaamini watatoa ushindani mkubwa tofauti na msimu uliopita.

“Tulikuwa na wachezaji wengi ambao si wazoefu kwenye ligi lakini kwa sasa usajili tulioufanya umezingatia kila sehemu iliyokuwa na upungufu kwenye maeneo husika, hivyo tunatarajia kufanya vizuri tofauti na msimu uliopita,” alisema kocha huyo.

Wachezaji wapya kikosini humo ni; Tausi abdallah, Neema Charles, Lucy Mrema, Mwantumu abdallah, Fatuma hassan, Fatuma Makusanya, hamisa hamis, happy hezron na amina ally bilali.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic