SAMATTA KUTUPA KARATA YA PILI DHIDI YA WABABE WA LIVERPOOL UEFA CHAMPIONS LEAGUE LEO
Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Mbwana Samatta, usiku wa leo akiwa na klabu yake ya KRC Genk anatarajiwa kushuka dimbani kwa mchezo wake wa pili wa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya (Champions League) dhidi ya Napoli.
Genk, itakuwa nyumbani Ubelgiji katika dimba la Luminus Arena ikiwakaribisha miamba kutoka Italia klabu ya Napoli.
Katika mchezo wake wa kwanza Genk iliangushiwa kichapo kizito cha goli 6-2 ugenini dhidi ya RB Salzburg, huku Samatta akifunga goli moja la kufutia machozi.
Katika mchezo huo, Samatta aliweka rekodi binafsi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Champions League na kufunga goli.
Napoli wao walianza kwa kuwafunga mabingwa watetezi Liverpool goli 2-0. Hivyo, Genk hii leo watakuwa tena na kibarua kizito cha kuwazuia Napoli.
Hata hivyo, Genk haijawahi kupata ushindi hata mechi moja ya Champions League katika mara zote tatu walizoshiri michuano hiyo, kwani wamefungwa mechi moja tu nyumbani kati ya sita walizocheza na kutoka sare tano.
0 COMMENTS:
Post a Comment