October 3, 2019


Kocha Mkuu wa Triangle United ya Zimbabwe, Tawarayi Mwangwiro ameibuka na kusema asingependwa kuoangiwa kucheza na Yanga katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika endapo atapangwa kundi moja na timu hiyo.

Droo ya nani na nani watacheza katika mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika Oktoba 9 mwaka huu baada ya Yanga kuondolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufungwa jumla ya mabao 3-2.

Mangwiro ambaye timu yake ilifanikiwa kuitupilia nje ya mashindano kwa kuifunga Azam FC katika mechi zote mbili, ameeleza kuwa na hofu na Yanga.

"Hakuna kitu ninachoomba kwa sasa kama kupangwa na Yanga, naiona ni timu nzuri ambayo ina Kocha mzuri.

"Katika timu zote zilizotolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika, naiona Yanga kama timu bora zaidi ya hii ya kwangu."

1 COMMENTS:

  1. Yaani kocha wa Triangle anaziogopa timu zilizotolewa mapema na wala sio zile zinazo au zilizoendelea kupambana mpaka zilizofika zilipofika. Hii haingii akilini. Huyo kocha anataka kuwazuzuwa wanaopenda kujisifu au kusifiwa na huku take moyoni

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic