IMERIPOTIWA kwamba mlinda mlango namba moja wa vinara wa Ligi Kuu England, Alisson Becker amerejea kwenye ubora wake.
Nyota huyo raia wa Brazil alikuwa nje ya Uwanja kwa wiki tisa baada ya kupata majeraha kwenye mchezo wa kwanza wa Premier League walipocheza dhidi ya Norwich City.
Mchezo huo Liverpool ilishinda mabao 4-1. Kurejea kwake kunaongeza matumaini ndani ya lango la Liverpool kuwa salama zaidi .
Adrian ambaye amesajiliwa msimu huu na Liverpool alichukua nafasi hiyo lakini alikuwa akifanya makosa mengi ya wazi ambayo yalikuwa yakiwakasirisha mashabiki.
Jurgen Klopp, Kocha wa Liverpool ambaye analisaka taji la Premier League baada ya kulikosa msimu uliopita amesema kurejea Kwa mlinda mlango huyo kutaongeza nguvu ndani ya kikosi chake.
Nyota huyo aliletwa duniani Oktoba 2,1992 Kwa sasa ana miaka 27 na msimu huu amecheza dakika 129 ambapo alicheza mechi ya ngao ya jamii dhidi ya Manchester City na mmoja wa ligi dhidi ya Norwich kabla ya kuumia.








0 COMMENTS:
Post a Comment