MCHEZO wa kirafiki leo uliochezwa mkoani Kigoma kati ya Simba na wageni wao Aigle Noir kutoka Burundi umekamilika kwa sare ya bila kufungana.
Mchezo huo umechezwa uwanja wa Lake Tanganyika jioni ya leo umeshuhudia mlinda mlango Beno Kakolanya akiendelea kuwa imara kwa kutoruhusu bao kupenya kwenye ngome yake tena.
Huu unakuwa mchezo wa pili sawa na dakika 180 kwa Kakolanya kukaa langoni kwenye mechi za kirafiki bila kuruhusu bao baada ya ule wa kwanza mbele ya Bandari kuokoa michomo minne ya moto.
Mpaka sasa Simba imecheza michezo mitatu na imeshinda miwili na imetoa sare mchezo mmoja leo mkoani Kigoma.
Pongezi kwa chama langu la simba ni mwaka mwingine was mafanikio
ReplyDeleteKampeni ondoa Manula inaendelea
ReplyDeleteANAEFANY VZR ANAPEWA NAFASI ACHA USHABIKI USIO NA MAANA
ReplyDeleteHAWA SI WALIFUNGWA NA NAMUNGO MTBWA NA AZAM PRE SEASON MNYAMA AMESHNDWA KUPATA USHND UDHAIFU MKUBWA
ReplyDelete