October 23, 2019



PAPY Tshishimbi nahodha wa timu ya Yanga amesema kuwa mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanja wa CCM Kirumba kuipa sapoti timu yao wakati itakapomenyana na Pyramids ya Misri kwenye mchezo wa kombe la Shirikisho.

Yanga jana ilifungulia vema mchezo wake wa kwanza ugenini kwa ushindi wa bao 1 lililopachikwa kimiani na Sadney Urknob akimaliza pasi matata ya Mapinduzi Balama.

Tshishimbi amesema kuwa:" Ni wakati wa mashabiki kuendelea kutupa sapoti,tuna kazi kubwa ya kufanya mbele ya Pyramids tunaamini utakuwa mchezo mgumu ila tupo tayari kwa ushindani,".

Msimu huu Yanga kwenye mechi zake mbili za kimataifa wakiwa nyumbani sawa na dakika 180 haijaambulia ushindi zaidi ya sare uwanja wa Taifa, itashuka tena uwanjani Jumapili ya Oktoba 27.

1 COMMENTS:

  1. USHAURI KUHUSU MAJERUHI WANAOONGEZEKA

    Tafadhali Rejea Kichwa cha Somo Hapo Juu

    Ushauri wangu ni kwamba idara ya Tiba na Utimamu wa Mwili na Wachua Misuli wafanye kazi usiku na mchana kuwarejesha mchezoni washambuliaji na walinzi na viungo tegemeo ambao watahitajika kwaajili ya mechi ya Jumapili. 

    Watu na Wapenzi wanaoifuatilia Yanga, wanauliza kwanini majeraha yanaongezeka kila kukicha?

    Inabidi uchunguzi wa kina ufanyike kwenye maeneo mengi tu nitayaorodhesha kama Ifuatavyo:

    ☑ Lishe ya Wachezaji...Namna ambayo Uongozi unavyo chukua Hatua kuondoa changamoto hizi kwa Kupata Utatuzi wa Kudumu
    ☑ Aina ya Mazoezi...Namna ambayo Uongozi unavyo chukua Hatua kuondoa changamoto hizi kwa Kupata Utatuzi wa Kudumu
    ☑ Tiba za Wachezaji.....Namna ambayo Uongozi unavyo chukua Hatua kuondoa changamoto hizi kwa Kupata Utatuzi wa Kudumu
    ☑ Ratiba za Wachezaji Kambini na Wasipokuwa Kambini...Namna ambayo Uongozi unavyo chukua Hatua kuondoa changamoto hizi kwa Kupata Utatuzi wa Kudumu
    ☑ Vifaa Vya Mazoezi na Vifaa Tiba Vilivyopo..Namna ambayo Uongozi unavyo chukua Hatua kuondoa changamoto hizi kwa Kupata Utatuzi wa Kudumu
    ☑ Viwanja Vya Mazoezi na Miundo Mbinu inayotumika......Namna ambayo Uongozi unavyo chukua Hatua kuondoa changamoto hizi kwa Kupata Utatuzi wa Kudumu!

    Ahsanteni na Nimatumaini Yangu haya yatawafikia Wahusika na yatafanyiwa Kazi na Wahusika

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic