MABINGWA
watetezi Simba, msimu huu mpya wametumia dakika 360 kutwaa tuzo tatu ambazo
zinatolewa na Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na
kufanya vema kwa wachezaji wao pamoja na Kocha Mkuu, Patrick Aussems.
Aussems
akiwa kwenye benchi la ufundi ameingoza timu yake kushinda mechi zote nne walizocheza
na kwenye mwezi Agosti, mshambuliaji Meddie Kagere aliibuka mchezaji bora
akiwashinda Luka Kikoti wa Namungo FC na Seif Karihe wa Lipuli FC.
Mwezi
Septemba tena zali liliwaangukia Simba ambapo safari hii walitwaa tuzo zote
mbili ikiwa ni ile ya mchezaji bora iliyokwenda kwa Miraj Athuman akiwashinda
Meddie Kagere wa Simba na Ismail Kada wa Polisi Tanzania.
Aussems alitwaa
tuzo hiyo aliwashinda Abdallah Mohamed ‘Bares’ Kocha Mkuu wa JKT Tanzania
pamoja na Adolf Rishard wa Tanzania Prisons.
Ndani ya
dakika 360 Simba imejikusanyia tuzo tatu ikiwa ipo kileleni na pointi zake 12
imefungwa mabao mawili pekee mpaka sasa, mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Azam
FC uwanja wa Uhuru, Octoba 23.
0 COMMENTS:
Post a Comment