October 19, 2019


Unakumbuka jinsi Yanga ilivyopangua fitna za watani wao Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam? Basi huko Mwanza mikakati thabiti imepangwa, ambapo itakuwa mara mbili zaidi ya ilivyokuwa awali, lengo ni kuhakikisha Mwarabu hatoki.

Kama ulikuwa hujui kilichotokea, basi ishu ilikuwa hivi, Simba walijipanga kuujaza Uwanja wa Taifa kwa kuingia mapema tangu asubuhi kwa lengo la kuwashangilia Zesco United ya Zambia katika mchezo wao dhidi ya Yanga hivi karibuni lakini Yanga wakashtukia na kutibua mipango.

Inaelezwa kuwa Yanga walitibua mipango hiyo kwa kufika mapema uwanjani siku ya mchezo huo mapema asubuhi na kulijaza jukwaa linalotumiwa na mashabiki wa Simba kwa kukaa wao ili kuwavuruga Wanasimba waliotaka kuwapa wageni nguvu kwa kuwashangilia.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo gazeti hili limezipata na kuthibitishwa na bosi mmoja wa juu klabuni hapo ni kuwa Kamati ya Utendaji ya Yanga imepanga kuwahi kufika Mwanza kwa ajili ya kuweka mipango ya ushindi kwenye mchezo huo.

Bosi huyo amesema wamepanga kupangua fitna za Simba walizozipanga kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza watakaoutumia kucheza mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids FC ya Misri kwa kuvamia na kukaa majukwaa watakayokaa watani wao hao.

Aliongeza kuwa, pia wamepanga kupeleka jezi 2,000 za Yanga ambazo kuanzia leo Ijumaa zitaanza
kupatikana kwenye Uwanja wa CCM Kirumba zitakazouzwa na wadhamini wao GSM kwa bei ya shilingi 35,000 na 25,000.

“Kama tulifanikiwa kupangua fitna za Simba kwenye Uwanja wa Taifa, Dar basi hatushindwi kuzipangua CCM Kirumba, Mwanza mkoa wenye mashabiki wengi wa Yanga.

“Hivyo, ni wakati sahihi kwa mashabiki wa Yanga wa Mwanza na maeneo ya jirani kujitokeza kwa wingi na mapema ili kuzima fitna za Simba walizozipanga, tumepanga iwe mara zaidi ya tulivyofanya Taifa.

“Tunataka uwanja mzima uwe na muonekano wa rangi ya kijani na njano, lengo ni kuwafunga Waarabu nyumbani,” alisema.

7 COMMENTS:

  1. Hakuna cha fitna wala mavi.Bebeni mzigo wenu .Mkufungwa8msirafute mchwi8.Mnaweka kiingilio elfu 10 halafu mnatafuta mchawi.Elfu 10 kiingilio cha chini??

    ReplyDelete
  2. Tatizo Yanga akili zenu zinawaza Simba tu badala ya kupambana na hali yenu.Soka la bongo hata halieleweki

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kweli tatizo la yanga akili zao zote na nguvu ni simba.Hii ndio inawavuruga yanga kisaikologia

      Delete
    2. Hapana,mawazo ya Yanga yapo kwa UD SONGO tuu na ndio maana wamebadili uwanja

      Delete
  3. Waafrika weupe hawana mchezo wanakula sana mlenda watawabamiza goli 5-0

    ReplyDelete
  4. Mtaruka sana lakini mkitua Chuma lazima kiingie.

    ReplyDelete
  5. Kumbe ndiyo mmana mmepanga kiingilio cha shs elfu 10 ili kuwskomesha mashabiki wa simba , kumbe mnatukomoa hata sisi maana mtego wa panya huingia na yule asiyekuwemo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic