October 19, 2019


Jose Mourinho anatarajiwa kuwa mchambuzi wa mchezo wa kesho Jumapili kati ya Manchester United dhidi ya Liverpool. Uamuzi huo umechukuliwa na kituo cha runinga cha Sky Sports ambapo baadhi ya mashabiki hasa wa United wameshangazwa na kuamini itakuwa ni nafasi ya kocha huyo kuendelea kuiponda United.

Mchezo kama huo ndiyo ambao ulisababisha United kumfukuza kazi Mourinho, Desemba mwaka jana baada Liverpool kushinda kwa mabao 3-1.

Timu hizo zinakutana huku kukiwa na presha kubwa kwa Kocha wa United, Ole Gunnar Solskjaer kutokana na matokeo mabaya ya msimu huu.

Inaaminika kuwa historia inaweza kujirudia kwa Solskjaer kupoteza kazi kama ilivyokuwa kwa Mourinho ikiwa timu yake itapata kipigo kikali kutoka kwa wapinzani wao wa jadi.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp anatarajiwa kuingiza kikosi kikiwa na nguvu kwa kuwa timu yake imekuwa ikifanya vizuri tangu kuanza kwa msimu huu licha ya kuwa mchezo utapigwa kwenye Uwanja wa Old Trafford ambao ni ugenini kwao.

Mashabiki wengi mitandaoni wametoa maoni ya kushangazwa na uamuzi huo wa Sky kumpa nafasi Mourinho kuchambua mchezo huo huku wale wa upinzani wa United wakifurahia kwa kuwa na hamu ya kusikia atakachozungumza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic