TFF YATOA TAMKO LINGINE JUU YA NDAYIRAGIJE KUPEWA STARS
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia Rais wake, Wallace Karia, limesema bado mpaka sasa halijatangaza Kocha Mkuu wa Taifa Stars.
Karia amesema kuwa watanzania hawapaswi kuwa na haraka juu ya kocha mpya bado kwani hawajamtangaza.
Kauli ya Karia imekuja mara baada ya kuelezwa kuwa kuwa kocha Mrundi, Etienne Ndayiragije ndiye atachukua rasmi nafasi hiyo baada ya kufanya vizuri akiwa na kikosi cha Stars tangu akaimu nafasi ya Emmanuel Amunike.
Karia amekanusha uwepo wa taarifa hizo akisema wao hawajazitoa na akiwataka watanzania wawe na subira.
"Sisi bado hatujamtangaza kocha wa Stars, watanzania wanapaswa kuwa na subira, kama Azam walisema ni wao na si sisi, subirini."








Sawa Mkuu
ReplyDeleteNgoja tuendelee kusubiri