October 20, 2019


Taarifa zinaeleza kuwa zinasema kuwa uongozi wa klabu ya Azam muda wowote wanatarajia kumtangaza Aristico Cioba kurejea kuifundisha timu hiyo.

Habari za ndani zinaeleza kuwa Azam wameamua kumrejesha Mromania Cioba ambaye alitumuliwa hivi karibuni baada ya kushindwa kufanya kile akilichotarajiwa.

Kocha wa sasa, Mrundi, Etienne Ndayiragije, inaelezwa ataachwa kutokana na mwenendo wake ndani ya Azam tangu atangazwe kuchukua nafasi hiyo.

Saleh Jembe Blog itaendelea kukujuza zaidi kitakachokuwa kinaendelea juu ya suala hilo.

3 COMMENTS:

  1. Ni ngumu kwa Azam kupata matokeo chanya kwa stahili hii ya kocha kuwa na vibarua viwili vya kazi.Ndayaragije achague kumtumikia mwajiri mmoja.Azam
    walikuwa na haraka ya kumfukuza kazi Hans Plujim.Na Azam mnapoamua kubadilisha benchi la ufundi inabidi pia kocha Iddi Cheche aondolewe vinginevyo mtakuwa mnatwanga maji kwenye kinu na kubadilisha makocha kila msimu.Chukulieni mfano wa Simba ilipoachana na Masoud Djuma ktk benchi la ufundi na tunaona kwa sasa kuna mambo chanya.Lingine ni kuhusu kocha Hans Pljuim kama aneomba kufundisha timu yetu ya taifa basi kwangu naona ni kocha sahihi kwani anayajua mazingara yetu ya soka na ni kocha makini.

    ReplyDelete
    Replies
    1. umenena vyema lkn kwa TFF hii hawataweza kumchukua pluign kwan tayari wamewaamini sana matola na Ndairagije, na Matola kama hujui ataanza kupiga majungu kwa Tff ju ya mkuu wake.
      pia Ndairagije anayochangamoto kubwa kuamua abaki wapi. ukweli ni kuwa anapaswa kufanya kazi kwa bosi mmoja, aone Yanga wanavyoyumba.

      Delete
  2. Ukweli ni kuwa si rahisi timu kupata mafanikio kwa stahili hii ya kocha Ndarayaigije na Zahera.Chukulia Simba licha ya wachezaji wake wengi kutumikia timu zao za taifa lkn zimenufaika na mazoezi/mechi za kirafiki na kumpa kocha mkuu na benchi lake kuelewa mapungufu yaliyojitokeza.Azam wanapaswa kujilaumu wenyewe kwa kunwachia kocha wao kutumikia mabosi wawili.Naiona Azam menejementi kupoteza muelekeo na wasipojiangalia Azam itabaki historian na kuziacha timu kongwe kuendelea kutamba.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic