UONGOZI YANGA WAFUNGUKA KUHUSIANA NA ISHU YA WAARABU KUGOMEA UWANJA
Uongozi wa Klabu ya Yanga umekanusha taarifa za wapinzani wao wa Kombe la Shirikisho Afrika (Caf), Pyramids FC ya nchini Misri kugomea kutumia Uwanja wa CCM Kirumba wa mkoani Mwanza.
Hiyo ikiwa ni siku chache tangu uongozi wa Yanga utangaze kuuhamishia mchezo huo CCM Kirumba utakaopigwa Oktoba 27, mwaka huu saa kumi jioni. Yanga, awali ilikuwa ikitumia Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam katika michezo ya Ligi ya Mabingwa Afrika kabla ya kuhamishia Mwanza.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Frederick Mwakalebela amelifunulia gazeti hili kuwa taarifa zinazodai wapinzani wao Pyramids kupeleka malalamiko Caf ikipinga mabadiliko ya uwanja waliyofanya siyo kweli.
“Hakuna malalamiko yoyote yaliyopelekwa na Pyramids, hivyo mchezo utachezwa Mwanza kama tulivyopanga awali, tunawafahamu wanaozusha hizo taarifa ni wapinzani hapa nchini.
“Ifahamike kuwa kabla ya kuanza mashindano kila timu ilitakiwa kuwasilisha viwanja viwili ambavyo watavitumia, sisi tuliwasilisha CCM Kirumba na Uwanja wa Taifa ambayo ndiyo viwanja rasmi kwetu,” alisema Mwakalebela.
Simba waliondolewa na UD Songo inawauma nini Yanga kuchezea mechi zao za Kimataifa Mwanza?
ReplyDeleteKila mkikwama kisingizio Simba .Mtachapwa tu hamna namna. Hata mpeleke Loliondo.
ReplyDeleteKusema ukweli viingilio ni vya juu sana angalau wangefanya kima cha chini 5,000 cha juu 50,000 lengo lisiwe mapato bali liwe ni kuujaza uwanja sasa sidhani kama kwa viingilio hivyo mtaujaza uwanja KWANI HII MECHI NI YA MUHIMU SANA KWA MAANA NYINGINE NAFASI NI MOJA TU KUSHINDA MECHI HII YA NYUMBANI HAKUNA NAFASI NYINGINE MSIFIKIRIE KWENDA MISRI KUSHINDA....USHINDI WENU NI KUUTUMIA UWANJA NA KUHAMASISHA MCHEZAJI NO. 12 AINGIE KUTOA HAMASA NA USHANGILIAJI. Halafu suala la vibali vya CAF watu wanachanganywa mlisema mmepokea barua ikiwaruhusu kuwatumia leo mnasema kanuni...sasa kwanini mliwapa matumaini watu kuwa watatumika halafu leo mmeyazima matumaini hayo?
ReplyDelete