October 14, 2019


Ni kama neema imeanza kurejea Yanga baada ya wachezaji wake Patrick Sibomana na Lamine Moro kuanza mazoezi jana katika Uwanja wa Polisi Dar es Salaam.

Wawili hao waliumia hivi karibuni jambo lililosabisha waondolewe katika programu ya Mwalimu sababu hawakuwa na utimamu wa mwili.

Kurejea kwa wachezaji hao kunazidi kutia nguvu kuelekea mechi ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho ambapo Yanga itakipiga dhidi ya Pyramids FC ya Misri.

Mbali na kurejea kwao, Yanga pia kama imeongezewa nguvu na CAF kufuatia wachezaji wake David Molinga na Mustafa Suleiman kuelezwa kupata vibali.

Molinga na Suleiman hawajacheza mchezo wowote wa kimataifa baada ya vibali hivyo kutia doa kwa kuchelewa kufika mapema.

4 COMMENTS:

  1. Lamine Moro hatacheza alionyeshwa kadi nyekundu vs Zesco yanga ilipokuwa katika harakati za kutaka kupindua meza ya chuma iliyokuwa inefungwa kwa nuts na bolts

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sasa sisi inatusaidia nn kama hatocheza Moro.usituchanganyie habari.

      Delete
    2. Kadi mbili za njano achakutuchanganyiaa habarii ss

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic