MICHEZO miwili ambayo Yanga imecheza msimu huu kimataifa uwanja wa Taifa haikuwa na matokeo mazuri jambo ambalo bado linamaanisha kwamba kuna kazi ya lazima inapaswa ifanywe.
Yanga ilianza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Township Rollers uwanja wa Taifa na ikakubali kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 ikiwa nyumbani na mashabiki zake.
Ilisonga mbele baada ya kushinda ugenini bao 1-0 ikaanza tena kama ilivyoanza awali kwa kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Zesco hapa kuna kazi kubwa ya kufanya.
Maana yake ni kwamba Yanga ikiwa nyumbani haijabadili mbinu za kutafutia ushindi ndio maana inaishia palepale ilipoanza ni wakati mpya kujipanga.
Kutupwa nje kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika na kuangukia kwenye Kombe la Shirikisho hapo kazi inaanza kuwa ngumu na kazi kubwa ni kutafuta ushindi.
Safari ya kwanza tena inaanza nyumbani ambapo Yanga itacheza na Pyramids ya Misri uwanja wa CCM Kirumba, bado inabaki kuwa ni nyumbani licha ya kubadili mkoa.
Rekodi hazina maana kubwa kwenye mpira licha ya kwamba zinapaswa zitazamwe ili kujifunza kwani kama mambo yamepita haikatazwi kurudia kujifunza.
Tunaona kwamba michezo mitatu ambayo imechezwa uwanja wa CCM Kirumba ya kimataifa Yanga ushindi wake umekuwa ni sare tu.
Wakati uliopo kwa sasa hauruhusu kulazimisha sare tena nyumbani kwani safari ikianza kusuasua mwanzo itakuwa ngumu kupindua meza kibabe kama ambavyo mara nyingi imetokea.
Maandalizi kwa sasa yanatakiwa kuwa makubwa kwenye ushindi pekee huku sare ikiwa ni bahati mbaya kwenu kufikiria.
Mashindano ya kimataifa ya sasa yapo wazi sana ila yana siri kubwa hasa kwenye mchezo wa nyumbani ambao huwa unakuwa umeshikilia matokeo ya ushindi.
Mwenye nafasi ya kupita hapa ni yule atakayetumia vema uwanja wa nyumbani na kupata matokeo chanya tofauti na yule ambaye atakuwa anasubiri kwenda kutafuta matokeo ugenini.
Hakuna mtihani mgumu kwa sasa ambao benchi la ufundi la Yanga unakumbana nao kama kupambana kupata matokeo chanya.
Wimbo wa sare mashabiki wameuimba sana mpaka imetosha kwa sasa wimbo mpya unaotakiwa ni ushindi nyumbani kisha ugenini huko mkipambana mkipata sare hata ushindi sio mbaya.
Ukweli ni kwamba msitegemee kwamba kutakuwa na kazi nyepesi hapana kitu kama hicho ngoma ni nzito na kila mmoja anahitaji matokeo chanya.
Wachezaji ni wakati wenu wa kuamua na kufanya kweli kwa kutoa burudani kwa mashabiki wenu ambao wanawapa sapoti kila mahali ambapo mnakuwa kwenye kazi.
Msifikirie kwamba mpo peke yenu bali Taifa linawaamini na linategemea kwamba mtafanya makubwa na yale ya kupendeza kwa ajili ya kupeperusha bendera ya Taifa.
Uzuri ni kwamba kazi inaonekana uwanjani na sio kwenye porojo za majukwaani kwani mpira ni mchezo wa wazi na yule ambaye atajiandaa atapata matokeo anayostahili.
Wakati wenu kuonyesha kwamba mmekomaa na mnaweza kubadili kile ambacho wengi wanafikira kwamba mtakwama mkiangukia pua nyumbani itakuwa ni kazi nyingine nzito kwenda kutafuta matokeo ugenini.
Mashabiki na watanzania kiujumla ni jukumu la kujitokeza kwa wingi uwanja wa CCM Kirumba kuwapa sapoti wawakilishi wetu wa Tanzania ambao wao wamebaki.
Hakuna ubishi ni Yanga pekee kwa Tanzania wapo kwenye mashindano ya kimataifa na dunia inawatazama kuona namna gani watafanya mbele ya wapinzani wao kutoka Misri.
Endapo akili za wachezaji zitafikira kushindwa basi hesabu zitakuwa zimefungwa jumla na hakuna ambaye atapata matokeo kwa kuwa wachezaji wameshajifunga.
Ila kama wachezaji wataamini ushindi upo mikononi mwao basi hicho ndicho kitakwenda kutokea watashinda na matokeo watayapata wakiwa kwenye ardhi yao ya nyumbani.
Muda mwingine ni vema kubadili kile ambacho kimekuwa kikiishi kwa wchezaji hasa mbinu ya mwalimu na kutafuta ushindi mapema huku mkitambua kwamba deni lenu ni kulilipa kwa mashabiki watakaojitokeza.
Kujitambua kwa wachezaji kutawafanya waaminiane na kila mmoja atimize majukumu yake kwa wakati ndani ya uwanja kutafuta ushindi.
Haya ni mawazo yako siyo ya wapenzi wala ya viongozi. Kaa nayo peke yako.
ReplyDelete