October 25, 2019


PASCAL Wawa, beki kisiki wa Simba amesema kuwa kilichowaponza wapinzani wao Azam FC kushindwa kupata matokeo mbele yao juzi kwenye mchezo wa ligi Uwanja wa Taifa ni kushindwa kuwa na utulivu jambo lililowafanya waziache pointi tatu kwao.

Simba ilicheza mchezo wake wa tano na kushinda kwa bao 1-0 ushindi uliowaweka kileleni wakiwa na pointi 15 na mabao 11 kibindoni.

Akizungumza na Saleh Jembe, Wawa amesema kuwa ulikiwa mchezo mgumu na wenye presha kutokana na timu zote kujuana mbinu na aina za uchezaji.

"Haikuwa kazi nyepesi kupata ushindi kwani wapinzani wetu wanatutambua nasi tunawatambua kitu kilichosababisha ugumu, tumepata matokeo hiyo ni furaha kwetu kutokana na utulivu wetu wao kiasi fulani walikosa utulivu.

'Hesabu zetu ni kuona tunapata matokeo mechi zote zinazofuata bila kujali tunapambana na nani kikubwa ni pointi tatu muhimu," amesema Wawa.

Mchezo unaofuata kwa Simba ni dhidi ya Singida United, Oktoba 27 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic