ZAHERA AGUNDUA NAMNA YA KUWAMALZA WAARABU MAPEMA KABISA CCM KIRUMBA
Kocha Mkuu wa Yanga Mkongomani, Mwinyi Zahera amesema njia pekee ya Yanga kutinga hatua ya makundi michuano ya Kombe la Shirikisho, ni kuhakikisha wanapata ushindi mnono nyumbani.
Oktoba 27, mwaka huu Yanga itashuka CCM Kirumba kumenyana na Pyramids FC kutoka Misri ukiwa ni mchezo wa raundi ya kwanza kusaka nafasi ya kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
“Mara nyingi timu za Tanzania zimekuwa na uwezo wa kupata matokeo hata kwa timu za Afrika ya Kaskazini (kwenye mechi za nyumbani) shida imekuwa mechi inapokuwa ugenini,”alisema Zahera.
“Ukishinda goli 1-0 nyumbani kwa timu za Kaskazini mwa Afrika unakuwa kama tayari umeshatoka,” alisema Zahera.
Katika hatua nyingine kiungo wa zamani wa Simba, Amri Kiemba amesema kuwa licha Pyramids FC kuwa timu isiyokuwa na uzoefu lakini Yanga wanahitaji umakini.
“Kwa tofauti ya Ligi ya Tanzania na Misri naona bado ni timu ngumu, haijalishi tunacheza na timu gani.
Tusiangalie historia ya timu tu, tuangalie pia historia ya ligi wanayocheza. Mechi haitakuwa rahisi,”aliongeza.
0 COMMENTS:
Post a Comment