Imeelezwa kuwa aliyekuwa Kocha wa Simba, Masoud Djuma, amejiunga na KMC FC ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Djuma amejiunga na KMC ikielezwa amesaini mkataba wa miezi sita ili kuitumikia timu hiyo ambayo ilikwa kwenye mwenendo mbaya tangu ichukuliwe na Jackson Mayanja.
Kocha huyo ametia kandarasi hiyo akitokea Bugesera FC inayoshiriki Ligi Kuu nchini Rwanda.
Ikumbukwe Mayanja ambaye ni raia wa Uganda, alifukuzwa siku chache zilizopita baada ya kushindwa kutimiza kilichokuwa kinahitajika.
Mtahangaika sanaaaa
ReplyDelete