November 14, 2019


Kijana James Otuma (53), katika Kijiji cha Lukume, Jimbo la Malava, Wilaya ya Kakamega nchini Kenya anashikiliwa na vyombo vya dola kwa ajili ya uchunguzi na mahojiano baada ya kumuua Mama yake aliyekuwa na umri wa miaka 65.

Mashuhuda wanasesema kuwa Kijana huyo mara kwa mara alikuwa akimtishia Mama yake na wamedai kuwa alikuwa ameathirika kwa uraibu wa Bangi na kwamba amekuwa akiwafanyia vurugu mara kwa mara.

Kisa cha mauaji hayo ni Kijana huyo kudai Mti uliopo kwenye nyumba ya Mama yake ni wake na anaweza kuamua kuukata siku akitaka, Mama yake alipokataa, Kijana huyo alichukua Panga na kumchinja.

Wananchi wenye hasira kali walijitokeza na kuanza kumshambulia kwa mawe kijana huyo aliyesemekana kuwa ana matatizo ya akili lakini polisi waliwahi kumuokoa kabla hajauawa.

Mwili wa marehemu umepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kakamega kwa ajili ya uchunguzi huku mtuhumiwa akishikiliwa katika kituo cha polisi cha Malava.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic