MIRAJ
Athuman ‘Sheva’ mshambuliaji wa Simba amesema kuwa anajifunza mambo mengi akiwa ndani ya Simba kutokana na kuwa na wachezaji wenye uzoefu.
Miraj amefunga jumla ya mabao manne ndani ya Simba akiwa na pasi moja ya bao amekuwa akifanya kazi kwa ukaribu na Meddie Kagere.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Sheva amesema kuwa masiha ndani ya Simba yamekuwa yakimpa somo kwa kucheza na wachezaji wenye uzoefu.
"Najifunza mengi nikiwa Simba hasa ukizingatia ninacheza na mchezaji Kagere ambaye ana uwezo mkubwa na uzoefu zaidi yangu, kwangu ni darasa na ninajifunza mengi," amesema Sheva.
Simba ipo nafasi ya kwanza ikiwa imecheza mechi 9 ina pointi 22 ikiwa imefunga mabao 16 na kufungwa jumla ya mabao matatu.
0 COMMENTS:
Post a Comment