BAD NEWS!! 15 WAFARIKI AJALI YA TRENI
Imeripotiwa kuwa takribani watu 15 wamefariki na wengine 58 wamejeruhiwa baada ya Treni mbili za abiria kugongana katika Wilaya ya Brahmnbaria Mashariki mwa Bangladesh Jumanne hii.
inaelezwa kuwa majeruhi wa ajali hiyo wamefikishwa katika hospitali tofauti tofauti zilizopo katika Mji huo. Aidha, wameongeza kuwa idadi ya watu waliofariki inaweza kuongezeka kutokana na baadhi ya watu kunasa katika viti vya treni hizo zilizopata ajali.
Kwa upande mwingine, usafiri wa treni katika Mji wa Dhaka, Sylhet na Chittagang umesimamishwa kwa muda ili kupisha zoezi la ukoaji kuendelea.
Rais wa Bangladesh Bw. Abdul Hamid na Waziri Mkuu Sheikh Hasima wameelezea masikitiko yao kufuaia tukio hilo. Aidha, usafiri wa Treni katika Miji ya Dhaka, Sylhet na Chittagang umesitishwa kwa muda
0 COMMENTS:
Post a Comment