November 15, 2019


Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Senzo Mazingisa ambaye ni raia wa Afrika Kusini leo, Alhamisi, Novemba 14, 2019, amefanya ziara ya kikazi katika ofisi za Kampuni ya Global Publisher inayochapisha magazeti bora nchini ya michezo ya Championi na Spoti Xtra.

Mbali ya magazeti hayo ya mengine ambayo siyo ya michezo ni Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Risasi, Amani na Uwazi.

Akizungumza katika ziara hiyo, Senzo amesema amepania kufanya makubwa ili kuipa Simba mafanikio makubwa ya Kisoka Afrika na duniani.

Katika ziara hiyo, Mazingisa akiwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Mulamu Ng’ambi walitembelea vitengo mbalimbali pamoja na kujionea shughuli za uzalishaji wa magazeti.

Lakini pia alitembelea katika studio ya Global TV Online pamoja na studio za +255 Global Radio kutazama namna ambavyo habari zinachakatwa na vituo hivyo kisha kurushwa kwa jamii.

Kujua zaidi mambo mengi aliyozungumza Senzo, nunua Gazeti la Championi leo Ijumaa, Novemba 15, 2019.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic