November 29, 2019


Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa mshambuliaji wao Obrey Chirwa atafunga mabao mengi msimu huu kwa kuwa tayari ameshaanza kuonyesha hali ya kujiamini ndani ya uwanja.

Chirwa juzi alianzisha safari ya kwanza kwa kufunga hat trick wakati Azam FC ikishinda mabao 5-0 dhidi ya Alliance FC kwenye Uwanja wa Nyamagana, huku mabao mengine yakifungwa na Idd Chilunda.

Cheche alisema kuwa, anaamini kwa mchezaji kuanza kufunga kunamuongezea hali ya kujiamini jambo litakalomfanya afunge mabao mengi msimu huu.

“Mwanzo alikuwa anasumbuliwa na hali ya kutojiamini akiwa uwanjani ila kwa kuwa ameanza kufunga basi tutarajie mwendelezo mzuri kwenye ligi na nina amini atafanya makubwa kwa kushirkiana na wenzake ukizingatia tuna mechi nyingi za kucheza,” alisema Cheche.

Chirwa anakuwa mchezaji wa tatu kufunga hat trick msimu huu kwenye ligi ya kwanza ilifungwa na Ditram Nchimbi mbele ya Yanga na ya pili ilifungwa na Daruesh Saliboko wa Lipuli FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic