November 29, 2019


Kocha ambaye jina lake likitajwa tu mashabiki wa Yanga wanashtuka, Mwinyi Zahera ametua nchini usiku wa kuamkia jana Jumatano.

Zahera tofauti na alivyozoeleka juzi alikuwa amepiga uzi mwekundu wa timu ya Taifa ya DR Congo na baadhi ya mashabiki waliokuwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere aliwagawia.

Yanga wamekuwa hawataki kumsikia Zahera kwa madai kwamba anavujisha siri zao kwenye vyombo vya habari.

Kwa mujibu wa gazeti la Spoti Xtra linajua kwamba kocha huyo ana ofa tatu mezani kwake ingawa amegoma kuweka wazi majina ya timu mpaka atakapomalizana na Yanga wiki ijayo.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic