SIMBA leo inashuka
uwanjani kumenyana na Ruvu Shooting ikiwa ni mchezo wake wa 10 rekodi zinaibeba
kutokana na matokeo chanya ambayo wameyapata kwenye mechi zake walizokutana
nyuma.
Tangu msimu wa 2016/17
Ruvu Shooting haijawahi kuambulia pointi hata moja mbele ya Simba zaidi ya
kupoteza mechi zake za ligi huku ikifungwa jumla ya mabao 20-1 kiujumla.
Zimekutana mara sita na
mechi zote zimechezwa uwanja wa taifa na katika mechi hizo sita mechi mbili
mashabiki wameshuhudia hat trick zikifungwa na Emmanuel Okwi 2017/18 na 2018/19
huku bao moja tu la penalti likifungwa na Meddie Kagere.
Mabao 21 yemefungwa
kwenye mechi sita huku Ruvu Shooting ikifunga bao moja pekee lililofungwa msimu
wa 2016/17 na Abdulahman Mussa aliyefunga bao hilo dakika ya 7 huku Simba
ikifunga jumla ya mabao 20.
Matokeo yao yapo namna
hii:-2016/17, Simba
2-1 Ruvu Shooting,
Ruvu 0-1 Simba, 2017/18, Simba 7-0 Ruvu, Ruvu 0-3 Simba, 2018/19, Ruvu 0-Simba 5, Simba 2-0 Ruvu Shooting.
Ruvu 0-1 Simba, 2017/18, Simba 7-0 Ruvu, Ruvu 0-3 Simba, 2018/19, Ruvu 0-Simba 5, Simba 2-0 Ruvu Shooting.
0 COMMENTS:
Post a Comment