AZAM FC leo ina kazi
kubwa mbele ya Mbao FC kuvunja mwiko wa kushindwa kupata pointi tatu mbele ya
Mbao FC uwanja wa CCM Kirumba kwa misimu mitatu mfululizo.
Azam FC iliyo chini ya
kocha mkuu, Arstica Cioaba raia wa Romania inamtegemea mshambuliaji wao Donald
Ngoma na Obrey Chirwa kuvunja mwiko huo wakati timu hizo zitakapomenyana.
Akizungumza na Saleh Jembe, Abdulkarim Amin ‘Popat’ ambaye ni mtendaji mkuu wa Azam
FC amesema kuwa mechi zote ni muhimu kwa
timu kupata ushindi huku kazi ya washambuliaji ikiwa ni kufunga tu.
“Tunakazi kubwa msimu
huu na kila mchezaji ana kazi ya kufanya kuanzia kwa mabeki mpaka washambuliaji
ikiwa ni pamoja na Ngoma na Chirwa wanatambua majukumu yao ya kufanya ndani ya
uwanja.
“Morali kwa wachezaji
ni kubwa na tunachohitaji ni kuona tunapata pointi tatu muhimu kisha hayo
mengine yatafuata kwani ligi ni ngumu na kila timu inahitaji ushindi,” amesema.
Azam FC kwenye mechi sita ambazo imecheza na Mbao imeshinda tatu pekee
na zote uwanja wao wa nyumbani Chamazi ilipokuwa CCM Kirumba imepoteza mechi moja
na sare mbili.
0 COMMENTS:
Post a Comment