November 11, 2019


ARTURO Vidal amekiri kuwa mchezaji mwenzake wa Barcelona, Antoine Griezmann ana wakati mgumu klabuni hapo tangu alipojiunga katika usajili uliopita akitokea Atletico Madrid.

Barcelona ilimnunua kwa dau la pauni milioni 108 nyota huyo ambaye bado hajaonyesha makali yake ndani ya klabu hiyo. 


"Imekuwa ngumu kwake kuendana na mazingira ya Barcelona kwa kuwa ni mapya kwake kwa sasa.

 "Ametua katika timu bora zaidi duniani ikiwa na wachezaji bora," amesema kiungo huyo raia wa Chile.

Griezmann aliifungia Atletico Madrid jumla ya mabao 94 katika mechi 180 kuanzia 2014-2019 inaelezwa kuwa Barcelona ina mpango wa kumuuza.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic