November 15, 2019




TAIFA stars leo imeanza vema michuano ya Afcon kwa kuibuka kidedea mbele ya timu ya Equatorial Guinea kwa kupata ushindi wa mabao 2-1 mchezo uliochezwa uwanja wa Taifa.


Stars iliyo chini ya Etienne Ndayiragije ilianza kwa kasi kipindi cha kwanza haikuweza kutumia vema nafasi saba za kipindi cha kwanza na kuruhusu wapinzani wao Equatorial Guinea kuandika bao la kwanza dakika ya 15 kupitia kwa Pedro Obiang liliwapeleka Stars mapumziko wakiwa nyuma kwa mbao huo uliofungwa nje ya 18.

Kipindi cha pili Stars ilianza kwa kulazimisha mashambulizi na iliwapeleka mpaka dakika ya 68 ambapo Simon Msuva aliandika bao la kwanza akimalizia pasi ya Mohamed Hussein 'Tshabalala' na kuweka mzani sawa.

Salum Abubakari alimaliza ile fujo isiyoumiza dakika 90 kwa kulipa mbao wa Obiang akiwa nje ya 18 kwa kuachia mshuti wake wenye uzito uliomshinda mlinda mlango wa Equatorial Guinea akimalizia pasi ya Ditram Nchimbi.

Ushindi huo unaifanya Stars kujikusanyia pointi zake tatu leo ikiwa kwenye uwanja wa Taifa.

4 COMMENTS:

  1. mhh ety noma wakati niwakawaifa2

    ReplyDelete
  2. Hongera stars tunawaxubiri libya kwao

    ReplyDelete
  3. Leo tumecheza kibabe tumepata matokeo mpaka kocha wao anasema game haikuwa fair kwao amesahau penalty tulizonyimwa sisi hadi anasema hawezi hata kuja mapunziko Tanzania. Hivi ndo inatakiwa sio tunacheza goigoi tunafungwa tunaishia kuitwa waungwana, mara nchi ya amani huku rohoni tunaumia. Tukiwa vitani tuwe kiaskari, Samatta ongeza ukakamavu. Tuliopangwa nao hawatishi zaidi ya kuwa mafundi wa fitna.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic