November 30, 2019


Kuvitengeneza: UGONJWA wa Ukimwi ni hatari na umeua watu wengi sana duniani. Leo tutazungumzia ugunduzi wa ugonjwa huu.

Mwanasayansi wa kwanza kutangaza kuwa ameweza kuviona Virusi Vya Ukimwi (VVU) ni mtaalamu wa Kifaransa, Dk Luc Montagnier.

Mtaalamu huyo ambaye aliongoza jopo la wanasayansi wengine katika taasisi ya Pasteur ya mjini Paris alitoa ripoti yake katika jarida la sayansi mwaka 1983.

Katika utafiti huo alihusisha virusi hao na uvimbe wa kwenye mashavu unaosababishwa na mafindofindo ambayo yalikuwa yanawaandama sana wagonjwa wa Ukimwi.

Hata hivyo, utafiti huo haukuweza kutoa picha halisi ya VVU hadi mwaka uliofuata mwanasayansi wa Kimarekani alipofanikiwa kukielezea kirusi hicho kwa sayansi inayoeleweka zaidi.

Mmarekani huyo, Dk. Robert Gallo akiongoza jopo la wanasayansi wengine, mwaka 1984 walitangaza ripoti yao ya utafiti kwa kina na kutoa machapisho manne ya ripoti kwenye jarida la kisayansi. Chakushangaza ni kwamba wapo wanasayansi wanaosema kwamba daktari huyo ndiye aliyetengeneza virusi vya ukimwi.

Kwenye jarida hilo alikielezea kirusi kinachosababisha Ukimwi kwa undani na namna kinavyoshambulia mfumo wa kinga.

Ripoti hizo baada ya kuchunguzwa zilionyesha wazi kuwa ndivyo ulivyo mfumo wa VVU hivyo mwaka 1986, Dk Gallo akatunukiwa tuzo ya Lasker.

Lasker ni moja ya tuzo za kisayansi zinazoheshimika duniani na ambayo imekuwa ikitolewa kwa watu waliofanya maajabu kwenye fani hiyo.

Tuzo hiyo ilimfanya Dk Gallo kupewa heshima ya juu zaidi katika tafiti zilizogundua VVU kuliko zile zilizofanywa na Wamarekani wenzake Dk Paul Volberding na Dk Marcus Conant, mwaka 1981 na ile ya Mfaransa Dk Luc Montagnier, mwaka 1983.

Tuzo hiyo ilionekana kumpa kichwa Dk Gallo kwani aliendelea kuchimbua zaidi VVU na kutoa ripoti mbalimbali ziliviweka wazi virusi hivyo na kuwapa picha halisi watafiti wengine duniani.

Moja ya utafiti huo ni ule alioutoa mwaka 1995 ulioonyesha kemikali iitwayo chemokines inaweza kusababisha VVU kushindwa kushambulia CD4 na hatimaye mwili unakuwa haufikii hatua ya kuugua Ukimwi.

Kwa namna Dk Gallo alivyoonyesha juhudi za kuchunguza VVU na Ukimwi, Mfuko wa Taasisi ya Bill Gate ilimpa Dola za Marekani 15 milioni sawa na zaidi ya Sh25.5 bilioni mwaka 2007 na hata miaka ya karibuni wameendelea kufadhiliwa.

Katika miaka hiyo ya 1980, walijitokeza wataalamu mbalimbali waliodai kuwa na dawa za kukabili Ukimwi.

Wakati huo kukiwa hakuna vipimo vya kubaini VVU, watafiti hao kutoka sehemu mbalimbali duniani, wakiwemo wa dawa za miti shamba, walikuwa wanatibu mtu ambaye tayari amekuwa anaugua Ukimwi.

Waliodai kuwa na dawa ni wale waliotibu dalili za ugonjwa kama vile kukonda, ngozi kuharibika, nywele kunyonyoka, vidonda kwenye koo na mdomoni.

Hata hivyo, kutokuwepo na vipimo vya haraka vya kuthibitisha mwathirika kama hana tena VVU, ilikuwa vigumu na mara nyingi walioonyesha kupona walionekana kurejewa tena ugonjwa na hata kupoteza maisha.

Mwaka 1985 Taasisi ya Chakula na Dawa ya Marekani (FDA) ilithibitisha kifaa cha kupima uwepo wa VVU kwenye damu.

Kipimo hicho ambacho hadi leo kimekuwa kikitumika ila kwa kuimarishwa zaidi, kwa kawaida kinapi ma uwepo wa chembe kinga maalumu inayotengenezwa na mwili baada ya VVU kuingia mwilini.

Kuwepo kwa vipimo hivyo kuliimarisha zaidi watafiti wa dawa kufanya kazi zao kwa uhakika zaidi katika kutafiti.

FDA ilitangaza AZT kuwa ni dawa ya kwanza ya ARV mwaka 1987. Mwaka huo pia ikatangaza aina ya kondomu iliyoimarishwa maalumu katika kuzuia maambukizi pale inapotumika kwa uangalifu.

Tangu wakati huo, ARV kadhaa zilitangazwa lakini zilizopo katika kiwango bora zaidi zilithibitishwa kati ya mwaka 1995 na 1996. Nyingi ya dawa hizo zimekuwa zikitumika hadi leo.

Utafiti mwingine umewezesha kuwapo kwa mchanganyiko wa baadhi ya dawa baada ya kuonekana zitakuwa na ufanisi zaidi.

MAKALA: Elvan Stambuli.

3 COMMENTS:

  1. Virus vilitengenezwa wakati wa vita baridi kuwauwa mashariki bahati mbaya madhara yakaanza marekani kwani homosexuality walilenngwa pia

    ReplyDelete
  2. Wazungu hasa wale wenye kuamini kuwa wao ndio wawe kuwa wataratibu wakuu na waendeshaji wa hii Dunia wapo tayari kufanya kufuru ya aina yeyote kuhakikisha kuwa wanakuwa juu ya masuala yote ya Dunia.Kihistoria aliemtoa Mchina shimoni ni Mrusi na hasa pale ambapo mchina ilipopokea zaidi ya wataalam millioni saba wa kirusi kuwafekea msitu wa kisiasa. Mataifa ya wazungu ambayo yamehusika sana na kuvamia mataifa mengine na kuyatawala na kupora watu na mali zao hayo ndiyo yanajiita mataifa ya kidekrasia.Na Taifa lolote litakalokwenda kinyume na Amri zao basi Taifa hilo litakuwa ni Taifa la kidikteta hata kama wananchi wake wanapata haki zao za msingi kuliko hata huko kwao .Na moja ya bara walilolinyanyasa na kuendelea kulinyanyasa ni Africa. Lakini cha kushangaza ni waafrica wenywewe wanaotumika kuiangamiza Africa. Angalia mfano hai wa Tundu Lisu na genge lake wanavyohangaika na kutumika kuimilikisha Tanzania kwenye mukono ya mabeberu hao wa Dunia. Kisa? Tundu Lisu alitaka kuuliwa? Lakini kabla ya tukio hilo la kutaka kuuliwa kwa Tundu Lisu? Alikaaje kaaje mpaka watu au watanzania wachukue uamuzi wa kutaka kuyaondosha maisha ya Lisu? Yeye Lisu hajawahi kusikia yakwamba watanzania kadhaa walikatwa vichwa vyao na hao anaowaona watu wa maana na kuvibeba na kuondoka navyo makwao? Ikiwa vijana wale weusi wachezaji mpira kule Ulaya ambao wengi wao hata wazee wao wamezaliwa Ulaya lakini bado wazungu hao wanaona kero kuwepo vipi yeye Lisu? Ndio anaona wanamuona mtu wa maana sana? Ukimwi nao wanasema umeanza Africa? Kweli? Ebola? Ni Africa pia? Africa ni jaa la wazungu na watu wake na rasilimali zake ni kwa ajili ya kuwanufaisha wao pia. Jaribio la dawa za kuua au kuponyesha binaadamu ambaye ni mzungu basi mwafrica ndie wa kujaribiwa.Mfano Ebola sio maradhi ni silaha za sumu za kibaolojia. Lakini vipi zilimfika mwafrica? Akili ni kwa wale waafrica wenye kujitambua.Ila kwa miaka ya hivi karibuni hapajawahi kutokea mtanzania mpumbavu kama Tundu Lisu na kama kuna watanzania wanaomuona mtu wa maana basi ni wapumbavu pia.kwani wazungu ni kwa ajili ya wazungu tu na waafrica ni kwa ajili ya kuwatumikia wao kwa ajili ya maslahi ya nchi zao mpaka Dunia hii inakwisha.

    ReplyDelete
  3. Kudos kwa comment nzuri Ebola ilipofika marekani na uingreza maana walipata walipokuwa Sierra Leone ilichukuwa miezi kadhaa waliwekeza mabilioni utafiti wakagundua chanjo ndio juzi imeletwa congo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic