November 13, 2019


MBWANA Samatta, nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania amesema kuwa morali ya wachezaji ni kubwa kuelekea kwenye mchezo wa kufuzu michuano ya Afcon Ijumaa Novemba 15 dhidi ya Equatorial Guinea.

Samatta amesema kuwa kazi ni ngumu kwa timu kutafuta matokeo ila kikubwa watafuata mbinu walizopewa na mwalimu kushinda.

"Haitakuwa kazi nyepesi kwani ushindani ni mkubwa, kila timu inahitaji ushindani nasi pia tunahitaji matokeo chanya.

"Mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti nasi tutapambana ndani ya uwanja ili yasijirudie ya msimu uliopita tulipolazimisha sare nyumbani," amesema.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic