DEOGRATIUS
Munish ‘Dida’ aliyekuwa mlinda mlango wa Simba kabla ya kutemwa kwa sasa
ameamua kujikita kwenye kilimo kazi ambayo alikuwa anaifanya kabla hajaja Bongo
kutafuta maisha.
Akizungumza
na Saleh Jembe, Dida amesema kuwa kwa sasa amejikita kwenye shughuli zake
nyingine mbali na soka kwani maisha lazima yaendelee huku akifikiria namna ya
kurejea kwenye soka la ushindani.
“Kikubwa
ambacho nakifanya kwa sasa ni masuala ya kilimo na hata nilipokuwa nyumbani
Kilimanjaro kabla sijaja Bongo nilikuwa ninalima na ninajua kazi ya shamba
vilivyo siwezi kudanganya na nimerejea hivi karibuni Bongo nikitoka shamba.
“Maisha ya
mpira yapo na ninatambua kuna majukumu mengine ambayo napaswa kuyafanya ikiwa
ni pamoja na kwenye timu ya taifa ya Beach Soccer (Soka la ufukweni) pamoja na
timu nyingine ambazo zinahitaji huduma yangu,” amesema Dida.
usikate tamaa mungu u pamoja nawe
ReplyDeleteRudi kucheza Moira kwani kipaji unacho
ReplyDelete