November 29, 2019


DEUS Kaseke, kiungo wa Yanga leo ameendeleza moto wake ndani ya Yanga baada ya kutengeneza pasi ya mwisho ya bao la ushindi lililofungwa na David Molinga akiwa ndani ya 18 kwa mguu wake wa kulia dakika ya 69.

Patrick Sibomana ndiye aliyefungua akauni ya mabao kwa Yanga akipachika bao la kuongoza dakika ya 25 baada ya mabeki wa Alliance kujichanganya na kumaliza kwa kufunga bao kwa mguu wake wa kushoto.

Bao pekee la kufutia machozi kwa Alliance lilifungwa na Juma Nyangi akiwa ndani ya 18 kwa kufunga bao hilo dakika ya 55.

Huu unakuwa ni ushindi wa pili kwa Yanga baada ya kutoka kushinda mbele ya JKT Tanzania mabao 3-2 huku Alliance ikiwa ni kichapo chao cha pili baada ya kutoka kufungwa mabao 5-0 na Azam FC uwanja wa Nyamagana.

4 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic