Kocha na mchezaji wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio' amemtaka Kocha Mkuu wa taifa Stars, Mrundi, Etienne Ndayiragije, kutoona aibu ya kumuanzisha benchi mshambuliaji Mbwana Samatta anayekipiga KRC Genk ya Ubelgiji.
Kauli ya Julio imekuja kufuatia Samatta kushindwa kung'ara juzi katiia mechi ya kuwania kufuzu AFCON dhidi ya Libya ambayo Stars ilipoteza kwa mabao 2-1.
Julio amesema Ndayiragije asiwe na hofu ya kumuanzisha benchi Samatta ili apate fursa na nafasi ya kuusoma vizuri mchezo ili aweze kufanya vema na aendane na timu vizuri.
"Inabidi Ndayiragije asione aibu kumuanzisha Samatta benchi ili ausome vizuri mchezo.
"Unaona kama mechi ya juzi alicheza lakini mechi ilikuwa imemkataa kabisa, ili kuepusha haya yanayotokea vema akawa hamwanzishi," amesema Julio.
Siyo mechi ya juzi tu imekuwa kawaida, Samatta anacheza chini ya kiwango akiwa anaitumikia timu ya taifa. Hata mechi ya juzi tulishinda Taifa bado hakucheza vizuri
ReplyDeleteKiwango cha Samata na hao wanaotakiwa kumchezesha kinafanana? Tatizo letu tunapenda keki huku tunamiliki vitumbua. Hakuna miujiza katika soka hata Brazil ya kina Romario ilikwama, Argentina ya Messi bado inahangaika na Messi wake na anajitoa vilivyo. Tazameni kariba ya wachezaji wanaomchezesha Samatta huko Genk kisha tufananishe na hawa wetu huku tukitazama na nafasi anayochezeshwa ndipo tuanze lawama na utaalamu wetu wa magazetini.
DeleteUmeongea vizuri washabiki wanataka Samatta afanye maaja kwa timu gani tuliyonauo
Deleteni kweli ,samata peke yake hawezi kufanya kitu,tusimtwike mzigo ... falsafa ya mpira ilivyo inategemea sana na mtu ambaye anaweza kumchezesha ili acheze
ReplyDelete