JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa hajaona kama kulikuwa na mazingira ya penalti wakati timu yake ikishinda mabao 3-1 mbele ya mabingwa watetezi Manchester City jana uwanja wa Anfield.
Klopp amesema kuwa wakati akitazama mpira alishtushwa na bao la mchezaji wake Fabinho alilolifunga akiwa nje ya 18 jambo ambalo hakutarajia lingetokea kwa muda huo kutokana na presha ya mchezo.
"Siwezi kuzungumza kama kulikuwa na mazingira ya penalti nilishtushwa na bao la Fabinho alilofunga akiwa nje ya 18 kabla ya Salah kufunga bao ambalo sijawahi kuliona akilifunga hivyo nawapongeza wachezaji kwa kujituma na kufunga bao la tatu kupitia kwa Sadio Mane," amesema.
Pep Guardiola Kocha wa City hakuwa na furaha na amesema kuwa walistahili kupewa penalti mbili kwenye mchezo huo uliowapa bao moja lililofungwa na Bernardo Silva.
Ushindi huo unaifanya Liverpool kuwa kileleni na pointi zake 34 huku City ikiwa nafasi ya nne na pointi zake 25.
0 COMMENTS:
Post a Comment