November 11, 2019


Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) limemfungia kwa miaka kumi (10) aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania Jamal Malinzi baada ya kumkuta na hatia ya matumizi mabaya ya fedha na kughushi nyaraka.

Mbali na adhabu hiyo, Malinzi pia amepigwa faini ya Dola za Kimarekani 503,000 ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 1.1 za Kitanzania.

Uamuzi huo umefanywa na Kamati ya Maadili ya FIFA baada ya uchunguzi uliobaini kuwa Malinzi alihusika katika matumizi mabaya ya fedha za FIFA (FIFA Financial Assistance Programme (FAP) funds), fedha za CAF, fedha nyingine za TFF pamoja na kughushi nyaraka za maazimio ya Kamati ya Utendaji ya TFF kati ya mwaka 2013 na 2017.


Adhabu hiyo inaanza kufanya kazi kuanzia Novemba 8, 2019 na tayari Malinzi mwenyewe ameshajulishwa.


“Kamati imemkuta na hatia ya kuvunja kanuni ya 24 inayohusu kughushi nyaraka, na kanuni ya 28 inayohusu matumizi mabaya ya fedha katika kanuni za maadili ya FIFA toleo la mwaka 2018 na hivyo inamfungia miaka kumi kujihusisha za shughuli zote za soka Kitaifa na Kimataifa”, imeeleza sehemu ya taarifa iliyotolewa leo na FIFA.

5 COMMENTS:

  1. Jamaa huyo ndo aliwapa yanga ubingwa mara 3 alafu wanajisifu eti mabingwa wa kihistoria fuck da shit

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani ukitoa hizo 3 simba ndio anakua bingwa wa kihistori

      Delete
  2. Mabingwa wa kihistoria mnazidiwa kila kitu na simba linapokuja suala la michuano ya kimataifa hiyo inaonyesha huo ubingwa wenu una maswali mengi juu yake mmeshiriki mara nyingi CAF lkn hamna rekodi yoyote ya ajabu sababu kule Awapo Ndolanga na Malinzi

    ReplyDelete
  3. Yanga ndio vigogo wa soka la Bongo, wengine wanaiga iga tu, ndio maana kelele haziishi.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic